Monday, August 10, 2026

THC BACK2SCHOOL BASH Sponsored by UTT‑Amis YAFANYIKA HOUSTON, TEXAS

Tanzania Houston Community Back2School Bash 2026 ya mwaka huu, iliyoandaliwa kwa ushirikiano na UTT‑Amis imekuwa moja ya matukio yenye mafanikio makubwa katika jumuiya ya Watanzania waishio jijini Houston. Tukio lilifanyika Jumamosi iliyopita katika viwanja vya George Bush Park, na liliwaleta pamoja watoto, wazazi, viongozi wa jamii na wadau mbalimbali kwa ajili ya kuunga mkono maandalizi ya wanafunzi kurudi shuleni.

UTT‑Amis kama mdhamini mkuu ilihakikisha kuwa kila mtoto alipata vifaa muhimu vya shule kama mabegi, vitabu, penseli, hadi vifaa vya usafi vikiakisi dhamira ya kuwekeza katika elimu na mustakabali wa watoto wa Diaspora. Tukio lilijaa furaha, michezo, muziki, chakula, na mazungumzo ya kujenga umoja, huku wazazi wakipata nafasi ya kuungana na viongozi wa jamii na kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuendelea kuimarisha ustawi wa familia.

Kwa ujumla, THC Back2School Bash 2026 imeacha alama ya upendo, mshikamano, na uwajibikaji. Ni mfano mzuri wa jinsi jamii inapoweza kuungana na wadhamini kama UTT‑Amis ili kuleta mabadiliko chanya kwa watoto na familia. Pata picha za tukio hilo hapa chini

Viongozi wa Tanzania Houston Community (THC) wakiwa na wawakilishi wa UTT-Amis

Rais wa Tanzania Houston Community Madam Leyla Kikuzi

Wanajumuiya wakipata darasa la uwekezaji kupitia UTT-Amis




































































































































 








No comments:

Post a Comment