Monday, August 10, 2026

THC BACK2SCHOOL BASH Sponsored by UTT‑Amis YAFANYIKA HOUSTON, TEXAS

Tanzania Houston Community Back2School Bash 2026 ya mwaka huu, iliyoandaliwa kwa ushirikiano na UTT‑Amis imekuwa moja ya matukio yenye mafanikio makubwa katika jumuiya ya Watanzania waishio jijini Houston. Tukio lilifanyika Jumamosi iliyopita katika viwanja vya George Bush Park, na liliwaleta pamoja watoto, wazazi, viongozi wa jamii na wadau mbalimbali kwa ajili ya kuunga mkono maandalizi ya wanafunzi kurudi shuleni.

UTT‑Amis kama mdhamini mkuu ilihakikisha kuwa kila mtoto alipata vifaa muhimu vya shule kama mabegi, vitabu, penseli, hadi vifaa vya usafi vikiakisi dhamira ya kuwekeza katika elimu na mustakabali wa watoto wa Diaspora. Tukio lilijaa furaha, michezo, muziki, chakula, na mazungumzo ya kujenga umoja, huku wazazi wakipata nafasi ya kuungana na viongozi wa jamii na kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuendelea kuimarisha ustawi wa familia.

Kwa ujumla, THC Back2School Bash 2026 imeacha alama ya upendo, mshikamano, na uwajibikaji. Ni mfano mzuri wa jinsi jamii inapoweza kuungana na wadhamini kama UTT‑Amis ili kuleta mabadiliko chanya kwa watoto na familia. Pata picha za tukio hilo hapa chini

Viongozi wa Tanzania Houston Community (THC) wakiwa na wawakilishi wa UTT-Amis

Rais wa Tanzania Houston Community Madam Leyla Kikuzi

Wanajumuiya wakipata darasa la uwekezaji kupitia UTT-Amis






Monday, August 11, 2025

BACK2SKUL2025 BBQ BASH PRESENTED BY THE THC GENTLEMEN CLUB

Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika Jiji la Houston, Texas na vitongoji vyake siku ya Jumamosi tarehe 09 August, 2025 katika viwanja vya Cullen Park walifanya party ya nyama choma (Back2Skul BBQ Party) . Party hiyo maalumu kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa shule kwa watoto wetu ilifanyika kwa udhamini wa Jumuiya ya THC wakishirikiana na Club ya Wakinababa wa Jumuiya (THC GENTLEMEN CLUB) . Pata picha nzuri za tukio hilo;

Rais wa Tanzania Houston Community Madam Leyla Kikuzi





Viongozi wa THC from L-R PR Cassius, President Leyla, Katibu Neema na VP Mvungi


Wednesday, November 20, 2024

MADAM LEYLA KIKUZI ACHAGULIWA TENA KUWA RAIS WA TANZANIA HOUSTON COMMUNITY

Siku ya Jumamosi tarehe 16 November, 2024 Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika Jiji la Houston Jimboni Texas walifanya uchaguzi wa Viongozi watakaoiongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha kuanzia January 1, 2025 hadi December 31, 2026.

Madam President Leyla Kikuzi

Katika uchaguzi huo Rais anayemaliza muda wake Madam Leyla Kikuzi ametetea kiti chake kwa kishindo baada ya kupata asilimia 99 ya kura zote zilizopigwa huku kukiwa hakuna mpinzani yoyote aliyejitokeza kuchukua fomu ili kuomba kuchaguliwa kuwa Rais.

Madam President Leyla Kikuzi akiapishwa na Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Bw. Nickson Mlay


Wanachama 42 walipiga kura online kupitia platform ya Jumuiya na wanachama 14 walipiga kura ukumbini. Katika jumla ya kura 56 zilizopigwa Madam Leyla alipata kura 55 za NDIYO na 1 ya HAPANA.

Safu nzima ya Uongozi wa THC (Executive Committee) ni kama ifuatavyo;

Madam Leyla Kikuzi - THC President 
Bw. Erasto Mvungi - THC Vice President 
Bi. Angela Christopher - General Secretary 
Bi. Zaina Daudi - THC Treasurer 
Bw. Cassius Pambamaji  - Public Relations 

Safu mpya ya Uongozi wa THC toka kushoto Bi . Angela Christopher
 (Katibu Mkuu) ,Bw. Erasto Mvungi (Vice President),
Madam PresidentLeyla Kikuzi na Bi. Zaina Daudi (Treasurer)


Madam President Leyla Kikuzi na timu yake waliapishwa siku hiyo hiyo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Nickson Mlay akiwa na kamati yake yote.

Uchaguzi wa Viongozi wa Bodi unatarajiwa kufanyika kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Jumuiya kwa mwaka 2025 utakaofanyika January.

Hongera sana Madam President Leyla Kikuzi na Team yako yote.

Friday, December 1, 2023

THE 5th THC KIDS & JUNIOR GALA 2023

THC - KIDS GALA ilifanyika Novemba 11, 2023. Event hii ya watoto ilikuwa na mafanikio makubwa. Iliwaunganisha watoto wa Jumuiya kuanzia umri wa mwaka 1 hadi umri wa miaka 16. Tunawashukuru sana Wanajumuiya wote waliotuunga mkono na wengi waliojitokeza kuleta watoto kwenye Event hii.

Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kila mtu aliyechangia kufanikisha Event hii wakiwemo Wafadhili wetu, Wanajumuiya waliojitolea na waliohudhuria. Usaidizi wenu ni ushahidi wa nguvu ya Jumuiya yetu na dhamira ya pamoja ya kuleta mabadiliko chanya.

Main Sponsor wetu alikuwa Ascend Cares Foundation

Donors wetu ni Wanajumuiya wote waliochangia pesa

Volunteers wote - Special thanks to the Kids Gala Committee 









CELEBRATING THE LIFE OF OUR BROTHER GEORGE KASAPIRA

Pata picha za shughuli ya kufurahia maisha ya Kaka yetu Marehemu George Kasapira hapa chini kwa hisani ya kaka Mtangazaji Maduhu

Pastor Lily, Beyonce na Ashanti (familia ya marehemu George)