Friday, March 10, 2017

TANGAZO LA UGONJWA WA KAKA HAJI RAJABU

Ndugu Wanajumuiya, 

Mwanajumuiya mwenzetu Bw. Haji Rajabu (Baba Luqman) amelazwa Medical Center ya Memorial Herman baada ya kuanguka na kupoteza fahamu jioni ya jana (Alhamisi March 09).

Bw. Haji alipelekwa ER ya West Houston na baadae akahamishiwa Medical Center kwa uchunguzi na matibabu zaidi.  

Kaka Haji Rajabu

Mpaka sasa brother Haji bado yupo ICU - Memorial Herman hospitali na yuko kwenye induced coma. Madaktari wa moyo wanachunguza kujua chanzo cha mshituko wa moyo wake na kumpatia tiba.

Mgonjwa anatakiwa kupumzika kwa hiyo madaktari wanashauri tusiende ICU kumuangalia kwa sasa mpaka hapo afya yake itakapotengemaa.

Familia itatoa taarifa na muongozo wa nini cha kufanya au msaada gani unaohitajika.

Tunaombwa tuendelee kumuombea katika sala na dua zetu.

No comments:

Post a Comment