Sunday, March 12, 2017

LATEST UPDATE AFYA YA KAKA HAJI

Ndugu Wanajumuiya, 

Tunashukuru mgonjwa ameamka na anaendelea vizuri. Asubuhi hii mgonjwa ameweza kuongea na ametoka kitandani na kutembea kidogo kwa msaada. Pia ameanza kukumbuka baadhi ya watu na matukio. 

Hiyo ni dalili nzuri na tumshukuru Mungu.

Tunaweza kwenda kumuona ingawa bado yupo ICU ya Heart and Vascular Institute pale Memorial Herman - Medical Center.

Anuani : 6411 Fannin St.   Houston, TX 77030. 
Chumba #806 
Ghorofa ya 8 (8th floor)

Tunaomba tuendelee kumuombea. 

Ahsanteni.

Uongozi THC
Kny Familia ya kaka Haji

No comments:

Post a Comment