Hello Wana-THC
Kwa mujibu wa Katiba yetu (Chapter IV, Article 20, Section I) tunapenda kuwajulisha kuwa Jumapili ya tarehe 09/11/2016 kuanzia 4:00pm – 8:00pm, tutakuwa na mkutano wa kuchagua Tume ya Uchaguzi katika ukumbi wa Hotel ya Houston Marriott Westchase 2900 Briarpark Drive, Houston, TX 77042.
Tume hiyo ya uchaguzi itakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi wa kugombea nafasi nne (4) za Wajumbe wa Board of Trustees ambao muda wao unamalizika pamoja na nafasi ya Katibu Mkuu wa THC ambayo ipo wazi baada ya aliyekuwa Katibu Ndg. Michael Ndejembi kujiudhuru nafasi hiyo.
Pia kama wanajumuiya wanataka kupendekeza mabadiliko yeyote ya katiba, tunawaomba wapeleke mapendekezo yao kwa Board of Trustees ili yajadiliwe , na baadaye kupelekwa kwenye mkutano mkuu kwa kujadiliwa zaidi na kupigiwa kura na mkutano mkuu.
Uchaguzi wa wajumbe wa Board of Trustees na Katibu unatarajiwa kufanyika wiki ya pili ya mwezi Novemba 2016.
Nawaomba mjitokeze kwa wingi.
Nawatakia siku njema
Neville Rugaimukam
Kny Board of Trustees
_.,_.___
Posted by: THCEC BOARD
No comments:
Post a Comment