Ndugu Wanajumuiya,
Habari za Mwaka Mpya.
Ni matumaini yetu kuwa wote tupo salama.
Tunapenda kuwafahamisha kuwa Uongozi wenu mpya wa THC kwa kipindi cha kuanzia Januari 2018 hadi Desemba 2019 umeanza kazi rasmi na makabidhiano ya nyaraka zote
muhimu za THC yamefanyika kwa amani na utulivu.
Katika kipindi hiki Uongozi wenu uko kwenye mchakato wa kuandaa Ajenda za Mkutano Mkuu wa kwanza wa mwaka wa Kikatiba wa THC ambazo tutazileta kwenu haraka iwezekanavyo.
Tunaomba ujumbe huu uwe kama utambulisho wetu kwenu na tupo tayari kupokea maoni au maswali kupitia barua pepe ya uongozi wa jumuiya : thcleaders@gmail.com (ambayo ndiyo njia pekee ya mawasiliano kwa sasa).
Ahsante sana
Imeletwa kwenu kwa niaba ya Uongozi na:
Lambert Tibaigana - THC President
No comments:
Post a Comment