Thursday, December 28, 2017

TAARIFA YA MAZISHI YA MTOTO GRAYSON ASMAN

Ndugu Wanajumuiya,

Kwa niaba ya familia ya Bw. na Bi. John Asman, tunapenda kuwajulisha kuwa mazishi ya mtoto wao Grayson Asman yatakuwa siku ya Jumamosi tarehe 12/30/2017.

Misa ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu itafanyika: 
Claire Brothers Funeral Home, 7901 Hilcroft Houston, TX 77081

Ratiba kamili ni kama ifuatavyo:

Kuaga mwili: 11:00am – 12:00pm 
Ibada: 12:00pm – 1:00pm

Baada ya zoezi hilo kukamilika, mwili wa marehemu utapelekwa kuzikwa katika makaburi yaliyopo Pearland anuani ni: Houston Memorial & Gardens 2426 Cullen Blvd Pearland TX 77581

Baada ya mazishi tutajumuika pamoja kwa ajili ya chakula, anuani ya mahali tutawajulisha hapo baadae.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Imetolewa:
Kamati ya mazishi kwa niaba ya wafiwa

No comments:

Post a Comment