Monday, February 18, 2019

MUUAJI WA ANDREW NICKY SANGA AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 35

Kesi ya Mtuhumiwa wa Mauaji ya ndugu yetu Andrew Nicky Sanga (Baba Zoe) imekamilika leo asubuhi hapa jijini Houston , Texas. Katika hukumu hiyo iliyosomwa na jaji mtuhumiwa Villere Henderson Johnson amehukumiwa kwenda jela kwa miaka 35 bila matarajio ya parole.

Familia ya Bw. Sanga inapenda kuwashukuru ndugu , jamaa , marafiki na Wanajumuiya wote kwa ujumla kwa kuwa pamoja nao katika kipindi chote hiki cha kufuatilia kesi ya mauaji ya kinyama ya mpendwa wetu .

"Tunapenda kuwafahamisha kuwa kesi imeisha rasmi leo ( 02/18/2019) saa 4 asubuhi kwa mtuhumiwa  kukiri makosa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 35 jela bila parole"- sehemu ya taarifa fupi kutoka kwa familia.

Tunamshukuru Mungu kwa sala zenu.


No comments:

Post a Comment