Tuesday, October 17, 2017

ZIARA YA MH. BALOZI WILSON MASILINGI JIJINI HOUSTON

Ndugu Wanajumuiya,

Tunapenda kuwafahamisha ujio wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mh. Balozi Wilson Masilingi ambaye anategemea kufanya ziara ya kikazi katika jiji letu la Houston mwishoni mwa wiki hii (Tarehe 20 hadi 21 Oktoba).



Madhumuni makubwa ya ziara hii ni kama yafuatayo:

i) Kuwapa pole wana-Houston na vitongoji vyake kutokana na madhara yaliyoletwa na kimbunga cha Harvey.

ii) Kukutana na kubadilishana mawazo na Watanzania wote kwa ujumla.

Tutawatangazia muda na sehemu ambako mkutano utafanyika.

Tafadhali mfahamishe na mwingine juu ya taarifa hii.

Ahsanteni sana.

Imetolewa na Uongozi wa THC

No comments:

Post a Comment