Thursday, September 8, 2016

THC-DSQUAD VS TANZANITE FC IN ATLANTA, GA

Timu ya soka ya Jumuiya ya THC - DSQUAD mwishoni mwa wiki ilisafiri hadi kwenye jiji wa Atlanta , GA kupambana na timu ya watanzania waishio katika jiji hilo maarufu kwa jina la Tanzanite FC. Matokeo ya mchezo huo uliofanyika katika viwanja vya Hammond Park yalikuwa ni 4-2 kwa wenyeji Tanzania FC. Magoli ya Tanzania yakifungwa na vijana machachari Abuu Mwasa na Andrew Francis. Timu hizi zinatarajiwa kurudiana wakati wa sherehe za Thanksgiving mjini Houston. Timu ya Dsquad inapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wote walioichangia katika kufanikisha safari yao ya Atlanta.

Kikosi cha DSQUAD 
DSQUAD safarini
Abuu Mwassa, Andrew Francis na Twaha Kambi

Wakongwe wa timu wakifanya warm ups

Captain Alune















No comments:

Post a Comment