Uongozi wa THC umepata ujumbe kutoka ofisi ya Ubalozi wa Tanzania zilizoko Washington DC kuwa unaandaa utaratibu wa kutuma muwakilishi kuja kushughulikia suala la kubadilisha Pasipoti (Passport Renewal). Hivyo basi Uongozi unaomba wale wote ambao wanahitaji huduma hiyo wawasiliane nasi kupitia email thc.leaders@gmail.com ili tuweze kupata idadi kamili kabla ya afisa Ubalozi kupanga tarehe ya kuja hapa Houston.
Zoezi hili linatakiwa kufanyika kwa haraka hivyo tunaomba wale wote wenye kuhitaji huduma hii wawasiliane na Uongozi THC mapema iwezekanavyo.
Ahsanteni sana
Imeletwa kwenu na UONGOZI
Tanzania Houston Community
No comments:
Post a Comment