Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika Jiji la Houston, Texas na vitongoji vyake siku ya Jumamosi tarehe 09 August, 2025 katika viwanja vya Cullen Park walifanya party ya nyama choma (Back2Skul BBQ Party) . Party hiyo maalumu kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa shule kwa watoto wetu ilifanyika kwa udhamini wa Jumuiya ya THC wakishirikiana na Club ya Wakinababa wa Jumuiya (THC GENTLEMEN CLUB) . Pata picha nzuri za tukio hilo;
Monday, August 11, 2025
Wednesday, November 20, 2024
MADAM LEYLA KIKUZI ACHAGULIWA TENA KUWA RAIS WA TANZANIA HOUSTON COMMUNITY
Siku ya Jumamosi tarehe 16 November, 2024 Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika Jiji la Houston Jimboni Texas walifanya uchaguzi wa Viongozi watakaoiongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha kuanzia January 1, 2025 hadi December 31, 2026.
![]() |
Madam President Leyla Kikuzi |
Katika uchaguzi huo Rais anayemaliza muda wake Madam Leyla Kikuzi ametetea kiti chake kwa kishindo baada ya kupata asilimia 99 ya kura zote zilizopigwa huku kukiwa hakuna mpinzani yoyote aliyejitokeza kuchukua fomu ili kuomba kuchaguliwa kuwa Rais.
![]() |
Madam President Leyla Kikuzi akiapishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Nickson Mlay |
![]() |
Safu mpya ya Uongozi wa THC toka kushoto Bi . Angela Christopher (Katibu Mkuu) ,Bw. Erasto Mvungi (Vice President), Madam PresidentLeyla Kikuzi na Bi. Zaina Daudi (Treasurer) |
Madam President Leyla Kikuzi na timu yake waliapishwa siku hiyo hiyo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Nickson Mlay akiwa na kamati yake yote.
Sunday, July 7, 2024
Sunday, June 2, 2024
Friday, December 1, 2023
THE 5th THC KIDS & JUNIOR GALA 2023
THC - KIDS GALA ilifanyika Novemba 11, 2023. Event hii ya watoto ilikuwa na mafanikio makubwa. Iliwaunganisha watoto wa Jumuiya kuanzia umri wa mwaka 1 hadi umri wa miaka 16. Tunawashukuru sana Wanajumuiya wote waliotuunga mkono na wengi waliojitokeza kuleta watoto kwenye Event hii.
Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kila mtu aliyechangia kufanikisha Event hii wakiwemo Wafadhili wetu, Wanajumuiya waliojitolea na waliohudhuria. Usaidizi wenu ni ushahidi wa nguvu ya Jumuiya yetu na dhamira ya pamoja ya kuleta mabadiliko chanya.
Main Sponsor wetu alikuwa Ascend Cares Foundation
Donors wetu ni Wanajumuiya wote waliochangia pesa
Volunteers wote - Special thanks to the Kids Gala Committee
CELEBRATING THE LIFE OF OUR BROTHER GEORGE KASAPIRA
Monday, November 13, 2023
Rest In Peace Kaka George Theodas Kasapira
OBITUARY
NOVEMBER 24, 1971 – NOVEMBER 8, 2023
IN THE CARE OF
Forest Park Westheimer Funeral Home and Cemetery
George Theodas Kasapira, age 51, of Houston, Texas passed away on Wednesday, November 8, 2023.
A visitation for George will be held Friday, November 17, 2023 from 3:00 PM to 7:00 PM at Forest Park Westheimer Funeral Home, 12800 Westheimer Road, Houston, TX 77077. A funeral service will occur Saturday, November 18, 2023 from 2:00 PM to 3:00 PM, 12800 Westheimer Road, Houston, TX 77077. A committal service will occur Saturday, November 18, 2023 from 3:00 PM to 3:30 PM at External Service Location, 12800 Westheimer Rd, Houston, TX 77077.
Fond memories and expressions of sympathy may be shared at www.forestparkwestheimer.com for the Kasapira family.