Wednesday, November 20, 2024

MADAM LEYLA KIKUZI ACHAGULIWA TENA KUWA RAIS WA TANZANIA HOUSTON COMMUNITY

Siku ya Jumamosi tarehe 16 November, 2024 Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika Jiji la Houston Jimboni Texas walifanya uchaguzi wa Viongozi watakaoiongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha kuanzia January 1, 2025 hadi December 31, 2026.

Madam President Leyla Kikuzi

Katika uchaguzi huo Rais anayemaliza muda wake Madam Leyla Kikuzi ametetea kiti chake kwa kishindo baada ya kupata asilimia 99 ya kura zote zilizopigwa huku kukiwa hakuna mpinzani yoyote aliyejitokeza kuchukua fomu ili kuomba kuchaguliwa kuwa Rais.

Madam President Leyla Kikuzi akiapishwa na Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Bw. Nickson Mlay


Wanachama 42 walipiga kura online kupitia platform ya Jumuiya na wanachama 14 walipiga kura ukumbini. Katika jumla ya kura 56 zilizopigwa Madam Leyla alipata kura 55 za NDIYO na 1 ya HAPANA.

Safu nzima ya Uongozi wa THC (Executive Committee) ni kama ifuatavyo;

Madam Leyla Kikuzi - THC President 
Bw. Erasto Mvungi - THC Vice President 
Bi. Angela Christopher - General Secretary 
Bi. Zaina Daudi - THC Treasurer 
Bw. Cassius Pambamaji  - Public Relations 

Safu mpya ya Uongozi wa THC toka kushoto Bi . Angela Christopher
 (Katibu Mkuu) ,Bw. Erasto Mvungi (Vice President),
Madam PresidentLeyla Kikuzi na Bi. Zaina Daudi (Treasurer)


Madam President Leyla Kikuzi na timu yake waliapishwa siku hiyo hiyo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Nickson Mlay akiwa na kamati yake yote.

Uchaguzi wa Viongozi wa Bodi unatarajiwa kufanyika kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Jumuiya kwa mwaka 2025 utakaofanyika January.

Hongera sana Madam President Leyla Kikuzi na Team yako yote.

No comments:

Post a Comment