Saturday, October 23, 2021

RATIBA YA MISA YA KUAGA MWILI WA KIJANA HUMPHREY MAGWIRA

Marehemu Humphrey Magwira

Ifuatayo ni Ratiba ya Kuaga mwili wa kijana wetu Humphrey Magwira.


Leo siku ya Jumamosi tarehe 23 Oktoba 2021, Wanajumuiya watapata wasaa wa kuaga mwili wa mpendwa Humphrey kuanzia saa saba kamili mchana (1:00pm) katika kanisa lifuatalo:

St Justin Martyr Parish, 13350 Ashford Point Dr. Houston, TX 77082 

Mipango ya kusafirisha mwili kuelekea Tanzania imeshakamilika. Familia inaendelea kutoa shukrani zao za dhati kwa ushirikiano wa hali ya juu unaoendelea kuonyeshwa na  Wanajumuiya wote wa THC, Umoja Church na community mbalimbali ambazo zinaendelea kutoa ushirikiano kwa Familia ya Mr. and Mrs Magwrira.

Baada ya kuaga mwili, familia ya marehemu inawakaribisha wote kwenye chakula cha pamoja kwa ajili  ya kutoa shukrani na kusherekea maisha ya Humphrey, kwenye anuani ifuatayo kuanzia saa kumi na nusu jioni (4:30pm):

Siena Hall:

11916 Bissonnet St, Houston ,TX 77099

Kina baba tunaomba mlete vinywaji ukumbini, tafadhalini na ahsanteni sana


Familia ya marehemu itaondoka siku ya jumapili tarehe 24 October 2021  (Baba/ Mama/ Kaka & Dada wa marehemu) ili kuwahi kuupokea Mwili Tanzania.

Mwili unatarajiwa kuondoka siku Jumatatu (October 25,2021) na kuwasili Tanzania siku ya Alhamisi tarehe 28, October 2021.

Mwili utaagwa na ndugu na jamaa wa Dar Es Salaam  siku ya Ijumaa tarehe 29 Oktoba 2021 na kuanza safari ya mwisho kuelekea Mahenge mkoani Morogoro ambapo mpendwa Humphrey atapumzishwa siku ya Jumamosi tarehe 30 Oct 2021.


Tuendelee kuwaombea wafiwa watakapokuwa safarini.

Ahsanteni sana na Mungu awalinde na kuwabariki kila mmoja wetu.


Imetolewa kwa niaba ya familia.

Bwana ametoa Na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe 

πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ

No comments:

Post a Comment