Friday, October 20, 2017

UPDATE - ZIARA YA MH. BALOZI WILSON MASILINGI JIJINI HOUSTON

Ndugu Wanajumuiya,

Kama tulivyowafahamisha hapo awali kuhusiana na ujio wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mh. Balozi Wilson Masilingi ambaye anategemea kufanya ziara ya kikazi katika jiji letu la Houston mwishoni mwa wiki hii (Tarehe 20 hadi 21 Oktoba).

Ifuatayo ni ratiba fupi ya ziara hiyo :

Mh. Balozi Masilingi anategemea kuwasili siku ya Jumamosi jioni ( tarehe 21 Oktoba). Baada ya kuwasili jioni hiyo Mh. Balozi atakuwa na kikao na viongozi wa Jumuiya ya THC  (EC na BOT)

Siku ya Jumapili (22/10) Mh. Balozi atakuwa na mkutano na Wanajumuiya wote katika Ukumbi wa Hotel Marriott uliopo kwenye anuani ifuatayo:

Marriott Hotel, 2900 Briarpark Dr. Houston, Texas 77042

Muda/ Time : 4pm - 7pm (saa kumi kamili jioni hadi saa moja usiku) 


Wote mnakaribishwa kwa wingi kuonana na kubadilishana mawazo na  muwakilishi wa serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ahsanteni sana.

Imetolewa na Uongozi wa THC

No comments:

Post a Comment