Wednesday, November 20, 2024

MADAM LEYLA KIKUZI ACHAGULIWA TENA KUWA RAIS WA TANZANIA HOUSTON COMMUNITY

Siku ya Jumamosi tarehe 16 November, 2024 Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika Jiji la Houston Jimboni Texas walifanya uchaguzi wa Viongozi watakaoiongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha kuanzia January 1, 2025 hadi December 31, 2026.

Madam President Leyla Kikuzi

Katika uchaguzi huo Rais anayemaliza muda wake Madam Leyla Kikuzi ametetea kiti chake kwa kishindo baada ya kupata asilimia 99 ya kura zote zilizopigwa huku kukiwa hakuna mpinzani yoyote aliyejitokeza kuchukua fomu ili kuomba kuchaguliwa kuwa Rais.

Madam President Leyla Kikuzi akiapishwa na Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Bw. Nickson Mlay


Wanachama 42 walipiga kura online kupitia platform ya Jumuiya na wanachama 14 walipiga kura ukumbini. Katika jumla ya kura 56 zilizopigwa Madam Leyla alipata kura 55 za NDIYO na 1 ya HAPANA.

Safu nzima ya Uongozi wa THC (Executive Committee) ni kama ifuatavyo;

Madam Leyla Kikuzi - THC President 
Bw. Erasto Mvungi - THC Vice President 
Bi. Angela Christopher - General Secretary 
Bi. Zaina Daudi - THC Treasurer 
Bw. Cassius Pambamaji  - Public Relations 

Safu mpya ya Uongozi wa THC toka kushoto Bi . Angela Christopher
 (Katibu Mkuu) ,Bw. Erasto Mvungi (Vice President),
Madam PresidentLeyla Kikuzi na Bi. Zaina Daudi (Treasurer)


Madam President Leyla Kikuzi na timu yake waliapishwa siku hiyo hiyo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Nickson Mlay akiwa na kamati yake yote.

Uchaguzi wa Viongozi wa Bodi unatarajiwa kufanyika kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Jumuiya kwa mwaka 2025 utakaofanyika January.

Hongera sana Madam President Leyla Kikuzi na Team yako yote.

Friday, December 1, 2023

THE 5th THC KIDS & JUNIOR GALA 2023

THC - KIDS GALA ilifanyika Novemba 11, 2023. Event hii ya watoto ilikuwa na mafanikio makubwa. Iliwaunganisha watoto wa Jumuiya kuanzia umri wa mwaka 1 hadi umri wa miaka 16. Tunawashukuru sana Wanajumuiya wote waliotuunga mkono na wengi waliojitokeza kuleta watoto kwenye Event hii.

Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kila mtu aliyechangia kufanikisha Event hii wakiwemo Wafadhili wetu, Wanajumuiya waliojitolea na waliohudhuria. Usaidizi wenu ni ushahidi wa nguvu ya Jumuiya yetu na dhamira ya pamoja ya kuleta mabadiliko chanya.

Main Sponsor wetu alikuwa Ascend Cares Foundation

Donors wetu ni Wanajumuiya wote waliochangia pesa

Volunteers wote - Special thanks to the Kids Gala Committee 









CELEBRATING THE LIFE OF OUR BROTHER GEORGE KASAPIRA

Pata picha za shughuli ya kufurahia maisha ya Kaka yetu Marehemu George Kasapira hapa chini kwa hisani ya kaka Mtangazaji Maduhu

Pastor Lily, Beyonce na Ashanti (familia ya marehemu George)







Monday, November 13, 2023

Rest In Peace Kaka George Theodas Kasapira

OBITUARY



NOVEMBER 24, 1971 – NOVEMBER 8, 2023

IN THE CARE OF

Forest Park Westheimer Funeral Home and Cemetery


George Theodas Kasapira, age 51, of Houston, Texas passed away on Wednesday, November 8, 2023.

A visitation for George will be held Friday, November 17, 2023 from 3:00 PM to 7:00 PM at Forest Park Westheimer Funeral Home, 12800 Westheimer Road, Houston, TX 77077. A funeral service will occur Saturday, November 18, 2023 from 2:00 PM to 3:00 PM, 12800 Westheimer Road, Houston, TX 77077. A committal service will occur Saturday, November 18, 2023 from 3:00 PM to 3:30 PM at External Service Location, 12800 Westheimer Rd, Houston, TX 77077.


Fond memories and expressions of sympathy may be shared at www.forestparkwestheimer.com for the Kasapira family.

Saturday, September 9, 2023

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA KIKATIBA

Ndugu Wanajumuiya, 

Uongozi wenu wa THC unapenda kuwatangazia kuwa Mkutano Mkuu wa Kikatiba utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 16/09/2023 (September 16th). Mkutano utafanyika katika anuani ifuatayo;

Venue/ Mahali : Holiday Inn Express, 2205 Baker Oaks Dr. Houston TX 77077 

Time/ Muda: 5pm to 9pm 


Ajenda za Mkutano ni kama ifuatavyo;

1) Bajeti

2) Ada ya Uanachama ( Membership Fees)

3) Mipango ya Jumuiya ( Community Plans/Goals)

4) Mengineyo


Wote mnakaribishwa katika Mkutano huu muhimu katika kuijenga Jumuiya yetu.


Kama kuna ajenda au maswali kabla na baada ya Mkutano tafadhali wasiliana na Uongozi kupitia baruapepe/email ya Community thc.leaders@gmail.com 


Ahsanteni sana,

Uongozi THC