Kwa mujibu wa madaraka yaliyokisimiwa na katiba, wanajumuiya kupitia mkutano mkuu wa tarehe 06/17/2023, ulipendekeza na kuchagua tume mpya ya uchaguzi na kuipatia madaraka ya kusimamia uchaguzi huru na wenye haki. Mkutano Mkuu uliwachagua wafuatao kuwa wasimamizi wa uchaguzi huo;
1. Anthony Rugimbana-Mwenyekiti
2. Sebastian Kassomi-Mjumbe
3. Lina Mwenda-Mjumbe
4. Goodluck Mbise-Mjumbe
5. Peter Mgema- Mjumbe
Tume iliendesha uchaguzi katika nafasi za Urais, Katibu, Mweka hazina na wajumbe 7 wa BOT kulingana na katiba yetu. Katika nafasi ya Rais wa jumuiya wagombea wafuatao walijitokeza kugombani nafasi hiyo;
1. Leyla Kikuzi
2. Issa Kingu
3. Seleman Kalinga( Sekhulu)
Mgombea mmoja alijitokeza kugombania nafasi ya Katibu wa Jumuiya;
1. Bernard Ngonyani.
Nafasi ya mweka hazina nayo ilipata mgombea mmoja pekee.
1. Zaina Oliver
Katika nafasi 7 za BOT, wagombea 8 walijitokeza kugombania nafasi hizo;
1. Lambert Tibaigana
2. Emmanuel Katili
3. Onesmo Fue
4. Sabhina Mwingira
5. Michael Ndejembi
6. Ephraim Mpendamani(Cash money)
7. Hamis Mtundy(Mpwa)
8. Augustine Mkude
Kwa kuzingatia maazimio ya mkutano Mkuu, tume iliendesha uchaguzi baada ya wanajumuiya 112 kukubali uchaguzi uendelee kufanyika siku ya tarehe 06/17/2023. Kati ya wanajumuiya 112 waliohudhuria, 95 walitumia haki yao ya msingi katika kushiriki upigaji wa kura na wanajumuiya 4 walitumia fursa yao ya online voting kupata haki yao. Jumla ya wapigaji kura ilikuwa 99.
Matokeo;
Baada ya zoezi la upigaji kura kuisha, wagombea wote waliombwa kuweka mawakala wao katika zoezi la uhesabuji wa kura. Yafutayo ni matokeo katika nafasi ya Rais wa jumuiya;
1. Issa Kingu- 38 uwanjani 4, online=42
2. Leyla Kikuzi. 47 uwanjani 0, online=47
3. Seleman Kalinga 10 uwanjani,0 online=10
Kamati ya uchaguzi, kupitia mamlaka ya mkutano Mkuu chini ya mwenyekiti Anthony Rugimbana, ilimtangaza Leyla Kikuzi kuwa Rais wa jumuiya katika kipindi cha 2023-2025 kulingana na katiba ya THC.
Nafasi ya Katibu Mkuu ilipata mgombea mmoja;
1. Bernard Ngonyani-84 uwanjani 3, online=87
Kamati ya uchaguzi, kupitia mamlaka ya mkutano Mkuu chini ya mwenyekiti Anthony Rugimbana, ilimtangaza ndugu Bernard Ngonyani kuwa Katibu Mkuu katika kipindi cha 2023-2025 kulingana na katiba ya THC.
Nafasi ya mweka hazina vile vile ilipata mgombea mmoja;
1. Zaina Oliver-89 uwanjani, 3 online=92
Kamati ya uchaguzi, kupitia mamlaka iliyopewa na mkutano Mkuu chini ya mwenyekiti wao Anthony Rugimbana, ilimtangaza ndugu Zaina Oliver kuwa mweka hazina katika kipindi cha 2023-2025 kulingana na katiba ya THC.
Yafuatayo ni matokeo ya uchaguzi wa nafasi 7 za wajumbe wa BOT katika kipindi cha 2023-2025;
1. Emmanuel Katili 65 uwanjani 0 online
2. Ephraim Mpendamani 69 uwanjani 0 online
3. Onesmo Fue. 70 uwanjani 0 online
4. Michael Ndejembi 60 uwanjani 0 online
5. Augustine Mkude 63 uwanjani 0 online
6. Lambert Tibaigana 72 uwanjani 0 online
7. Sabhina Mwingira 56 uwanjani 0 online
8. Hamis Mtundy. 41 uwanjani 0 online
Kulingana na matokeo hayo, kamati ya uchaguzi kupitia mamlaka iliyopewa na mkutano mkuu chini ya mwenyekiti Anthony Rugimbana, ilitangaza majina yafuatayo kuwa wajumbe wa BOT katika kipindi cha 2023-2025 kulingana na katiba ya THC.
1. Lambert Tibaigana
2. Onesmo Fue
3. Ephraim Mpendamani
4. Emmanuel Katili
5. Augustine Mkude
6. Michael Ndejembi
7. Sabhina Mwingira
Kamati ya uchaguzi imependekeza mkutano ujao ujadili kwa kina kuhusu nafasi 3 BOT ambazo huwa zinafanyiwa uchaguzi kila baada ya miaka 2 ili utaratibu tuliojiwekea kulingana na katiba yetu uweze kufanya kazi vizuri.
Kamati ya uchaguzi ilimtaarifu Rais mteule ndugu Leyla Kikuzi azimio la kupewa siku 7 ili aweze kuunda timu yake yenye makamu wake na msemaji mkuu wa jumuiya kabla ya zoezi la makabidhiano na kuapishwa halijafanyika.
No comments:
Post a Comment