Ndugu wana THC,
Natumaini wote tupo salama. Naamini wote tunajua kuna Excutive Order kuhusu sheria za uhamiaji zinazoendelea nchini ambayo imeleta utata, confusion, stress miongoni wetu n.k
Kwasababu ni mambo ya kisheria na wanajumuiya wetu wanamahitaji mbalimbali tumeona tutafute wataalaamu wa sheria za uhamiaji ili kuja kuongea na sisi.
Tumepata Mwanasheria ambaye ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Houston Prof. Susham M. Modi aliyebobea kwenye sheria za uhamiaji ( Immigration Law ) amekubali kukutana nasi siku ya Jumapili mchana saa nane kamili ( tarehe 12 February 2017.
Uongozi ( chini ya Vice President Lambert Tibaigana) unafuatilia mipango ya ukumbi mtajulishwa pindi mipango itakapokamilika.
Tunaomba haya yafuatayo kwa yeyote atakayeshiriki:
1: Kujiandikisha jina kwenye email ifuatayo :
donaldsexecutiveorderqanda@gmail.com
ili kuweza kuweka nafasi na viti (seats) kutokana na wahudhuriaji.
2: Kwa mtu mwenye swali/ maswali kutuma ili tuweze kumtumia ikihitaji majibu ya kisheria awe ameyandaa.
Follow up questions zitaruhusiwa na maswali ya papo kwa papo - ila ni vyema kutuma maswali kwa lugha yeyote kwa email iliyotajwa hapo juu.
Professor Susham M. Modi Biography :
Received a B.A., magna cum laude, from the University of Texas at Arlington and a J.D. from Penn State Law School.
Experience & Accolades
* Adjunct Professor of Law at the university of Houston Law Center
* Previously worked at Harvard Law School
* Has won several immigration cases
* Rated Top 2014 and 2015 Houstonia Magazine's Lawyer
Tunashukuru sana kwa ushirikiano - tujiandikishe kwa ajili ya maandalizi mazuri.
Zoezi zima limeratibiwa kwa niaba ya Uongozi wa THC na:
VP Lambert Tibaigana
No comments:
Post a Comment